Nyumbani

Mtwara wawaza kuunda timu ya soka

WANANCHI na wadau mbalimbali mkoani Mtwara wametakiwa kujitoa kwa ajili ya kuanzisha timu ya mpira wa miguu itakayopewa jina la Mtwara kwa lengo la kushiriki michuano mbalimbali.

Haya yaeelezwa baada ya uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mtwara (MTWAREFA).

Mwenyekiti wa Chama hicho Athumani Kambi amesema chama cha mpira pekee hakiwezi kupata timu kwenye ligi kuu bila ya umoja wa wadau serikali kuweka nguvu na wananchi kwa ujumla.

“Timu ya ligi kuu haipo kweli kwasababu timu iliyokuwepo ilikuwa Ndanda nayo sasa hivi haipo kabisa”

“Ilikuwepo timu ya Mbeya Kwanza nayo ilikuja kwa kuhamia hatujui kama mwaka huu itakuwepo lakini kama itakuwepo tutajaribu kuisaidia na kuhakikisha inakwenda kwenye ligi kuu,” amesema Kambi

Amesisitiza kikubwa wananchi wa Mtwara wajitoe tuanzishe timu nzuri tuiendeshe kwa jina la Mtwara wote kwa pamoja kama walivyokuwa wanafanya wenzetu wa Tabora Mbeya”

Amesema sehemu zingine huwa wanafanya vizuri kwani wanachukua timu moja hata kwa kwenda kuinunua na kuleta kwenye mikoa yao kuifanyia kazi na inaenda kupanda ligi kuu.

“Bila umoja bila kupata wadau, msaada mkubwa kutoka serikalini hatuwezi kupata timu kwenye ligi kuu”

Hata hivyo amewataka viongozi wa vyama shiriki ambao ni wenyeviti kuacha kuwaondoa watu kwenye vyeo vyao bila kufata katiba na taratibu.

Amefafanua zaidi kuwa, katiba inampa mwenyekiti mamlaka ya kumpendekeza katibu kwenye kamati ya utendaji na kwenye kumtoa afate utaratibu huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa wanawake mkoani humo, Zuhura Nandala amesema kumekuwa na changamoto ya kutokuchezwa kwa ligi za wanawake hususani wilayani hivyo amewaomba viongozi wa FA ambao ni walezi kwenye ngazi za wilaya kwenda kusimamia ligi za wanawake.

Lameck Nyambaya Mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es salaam ambaye pia ni mwakilishi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) meipongeza Mtwarefa kwa kuendelea kufata katiba.

Aidha amewataka wote kwa pamoja kuacha makundi na badala yake waendelee kushirikiana baada ya uchaguzi huo ili waweze kupata timu ligi kuu.

Leo Juni 29, 2024 (MTWAREFA) kimefanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti ambae ni Athumani Kambi aliyepita bila kupingwa.

Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na wajumbe wawili wa kamati tendaji ni Salum Telela na Majid Mkwayaya.

Related Articles

Back to top button