Habari Mpya

Ngao ya jamii yampa mwanga kocha Vital’o dhidi ya Yanga

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Vital O ya Burundi, Sahabu Parris amesema dakika 180 alizowasoma Yanga zimempa mwanga wa jinsi gani ya kumuingia mpinzani wake katika mchezo wa awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Amesema ametumia dakika 90 katika michezo miwili kuwasoma kuona ubora na madhaifu ya Yanga walipocheza dhidi ya Simba na Azam FC, nusu na fainali ya Ngao ya Jamii

Kesho Jumamosi August 17 Yanga itatupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Vital’o ya Burundi, uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Kuelekea mchezo huo, Kocha Parris amesema wamekisuka vyema kikosi chake kwa maandalizi anategemea kupata ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.

“Niliwasoma Yanga, kwenye mechi mbili walizocheza nimeona ubora na madhaifu yao, siwezi kusema wako bora sehemu gani, nitajua mbinu gani nitaitumia kupata ushindi,” amesema Parris.

Ameongeza kuwa katika mpira wa sasa hakuna nyumbani wala ugenini, anachoangalia zaidi ni jinsi walivyofanya maandalizi waliyoyafanya kwa ajili ya kupata ushindi.

Related Articles

Back to top button