Bundesliga

Bundesliga yatawala msimamo UCL

MUNICH UJERUMANI: KLABU kutoka katika ligi dume barani Ulaya ligi kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga zimetawala msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyokuja na sura mpya baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza kati ya 8 inayotarajiwa kupigwa siku za usoni.

The Bavarians Bayern Munich ndio vinara katika msimamo huo wakiwa na pointi 3 na faida ya kuwa na magoli mengi baada ya kuikaanga Dynamo Zagreb 9-2.

Katika 8 bora wapo pia mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayer Leverkusen katika nafasi ya 3 na Borussia Dortmund katika nafasi ya 5.

Kutoka Laliga ya nchini Hispani, Mabingwa watetezi wa UCL Real Madrid wamejificha katika upande wa pili wa msimamo huo wakiwa nafasi ya 8 na pointi zao 3. Huku mahasimu wao FC Barcelona wakikamatilia nafasi ya 22 baada ya kichapo cha 2-1 kutoka kwa AS Monaco hapo jana.

Farasi waliomaliza nafasi mbili za juu katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya England mabingwa Manchester City na nafasi ya pili Arsenal walishindwa kufurukuta wote wakitoa sare ya 0-0 matokeo yanayowafanya kuwa nafasi ya 16 Arsenal na 20 Manchester city.

Mbeba maono wa ligi kuu ya England amekuwa Aston Villa ambaye amerejea katika michuano hiyo baada ya takriban miaka 40 akikaa katika nafasi ya 4. Jogoo wa jiji nae hajalitia aibu taifa, ushindi wa mabao 3 – 1 ugenini dhidi ya AC Milan unamuweka katika nafasi ya 7.

UEFA champions league inatarajiwa kuendelea kwa mzunguko wa pili kuanzia October 1 mwaka huu huku mechi za kusisimua zinazotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi ni pamoja na

Arsenal vs PSG

Bayer Leverkusen vs AC Milan

Dortmund vs Celtic

Aston Villa vs Bayern Munich

RB Leipzig vs Juventus.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button