Masumbwi

Nasibu Ramadhani, Juma Choki kukiwasha Dar Boxing Derby

DAR ES SALAAM: MABONDIA 12 wa ngumi za kulipwa nchini watapanda ulingoni katika pambano la ‘Dar Boxing Derby’, linalotarajiwa kufanyika Juni 29, mwaka huu, Viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini hapa.

Mratibu wa pambano hilo, Seleman Semenyu ametaja mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo, Nassib Ramadhani dhidi ya Juma Choki pambalo la uzani wa 59 Kg la raundi 8, ikiwa ni mara ya kwanza mabondia hao kukutana kila mmoja akiwa na rekodi nzuri katika mchezo huo.

Mara ya mwisho Nassib alipanda ulingoni na kumchapa kwa pointi mpinzani wake Immanuel Naidjala, raia wa Namibia, Machi Mosi mwaka huu, ukumbi wa Werehouse, Masaki.

Semunyu amesema mandalizi yanaendelea, anaimania yatakuwa mapambano ya kuvutia kwa sababu kuna baadhi ya mabondia ni mara ya kwanza kukutana.

“Kila kitu kipo sawa, mabondia wapo kambini wanajiandaa, tunaimani itakuwa pambano nzuri na kuvutia wapenzi wa mchezo huu kwa sababu kuna Nassib na Choki ni mara ya kwanza kukutana na wote mabondia wazuri,” amesema Semunyu.

Ameendelea kuwataja mabondia ambao watasindikiza pambano hilo ni
Tonny Rashid dhidi ya Oscar Richard uzani wa 84Kg, Saidi Mkola dhidi ya Saidi Bwanga uzito wa 58Kg, Loren Japhet atazichapa na Issa Nampepeche, Charles Tondo atapanda ulingoni dhidi ya Haidary Mchanjo, Kassim Hamad dhidi ya Gabriel Moris.

Ramadhani Bonny atapanda ulingoni dhidi ya Adam Ngange, Gabriel Chola atanyukana na Frank Nampumula, Fred Sebastian dhidi ya Barnaba Alexender, Shazi Hija na Ibada Jafary na Peter Damian na Rajab Chanda kwa wanawake Najma Isike dhidi ya Nasra Msimi katika uzito wa 61 kg raundi ya sita.

Related Articles

Back to top button