“Nafasi ya 5 UCL haitupumbumbazi” – Nuno

Nottinghamshire, Bosi wa Nottingham Forest, Nuno Espírito Santo amesema kuongezeka kwa nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kutoka nafasi 4 hadi 5 hazitawapumbaza na badala yake watakaza uzi kuhakikisha wanakaa kwenye nafasi ya kufuzu Ligi hiyo.
Forest walio nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi point 5 mbele ya mabingwa watetezi Manchester City watakuwa nyumbani kuwakabili majirani wa Liverpool, Everton katika harakati za kuendelea kujiimarisha kuelekea kutimiza ndoto yao ya kucheza Champions League kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1980/81 na kocha nuno anasema hatapumbazwa.
“Iko mikononi mwetu, inafungua fursa zaidi za ushindani lakini kwetu haina maana yeyeote. ‘approach’ yetu itakuwa ile ile. kila siku tutaandaa wachezaji kwa kila mchezo hatutapumazwa na hilo kwa sababu tayari tupo kwenye njia ya kutimiza jambo kubwa” Amewaambia Wanahabari kwenye mkutano kuelekea mchezo wa Everton.
Sambamba na hilo Nuno ameonesha wasiwasi juu ya majeraha yanayokinyemelea kikosi chake kwani amekuwa bila mfungaji wake bora Chris Wood tangu alivorudi majeruhi aliyoyapata akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa huku wenzake Taiwo Awoniyi, Ola Aina na Anthony Elanga wakistrago na masuala ya ‘Fitness’