EPL

Akanji aona mwezi Man City

MANCHESTER: BEKI wa kati wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Manuel Akanji amesema anaamini sare waliyoipata hapo jana dhidi ya ya Everton inaweza kuwa mwanzo wa nyakati nzuri ndani ya klabu hiyo.

Akanji ameiambia AFP kwamba tofauti na michezo mingine mchezo huo dhidi ya Everton umeonesha wanaweza kufanya kitu kubadilisha mwenendo mbaya wa klabu hiyo katika siku za hivi karibuni.

“Haikuwa siku nzuri lakini ukilinganisha na michezo mingine, tulicheza vizuri sana kuanzia mwanzo hadi mwisho, tulijaribu kufunga mabao, tulicheza mchezo wa kushambulia lakini Everton walikuwa na bahati, tulitaka kushinda lakinj haikuwa bahati yetu”

“Tunahitaji kuendelea kupambana na fursa nyingine iko mbele yetu, hatutaki kitu kingine tunataka ushindi hatuna cha kufanya lakini naamini tutarejea kwenye namna yetu ya uchezaji hivi karibuni tunafanya kila kitu” amesema Akanji

Manchester City watakuwa wageni wa Leicester City hivi karibuni huku matokeo ya mchezo dhidi ya Everton yanawafanya vijana hao wa Pep Guardiola kushinda mchezo mmoja pekee katika 13 waliyocheza huku wakiwa nyuma kwa pointi 14 nyuma ya vinara Liverpool ambao bado wana mchezo mkononi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button