EPL
Doku: Nilinipata tabu sana

MANCHESTER:Winga Mbelgiji wa klabu ya Manchester city Jérémy Doku ameweka wazi kuwa alipata tabu kuzoea mazingira ya klabu hiyo hususan lugha na Lafudhi ya baadhi ya wachezaji wenzake wa Manchester city.
Akizungumza kwenye mahojiano na Ben Foster wa Prime video sport Doku amesema alipata tabu kuwaelewa baadhi ya wachezaji aliokuwa nao karibu kama Phil Foden na Jack Grealish.
“nilipata tabu kidogo na baadhi ya lafudhi hivyo sikuweza kuelewa kila kitu, kwa mfano Phil akiongea inakuwa ngumu sana kuelewa. Jack ni mcheshi sana lakini sikuwa naelewa kila alichonitania” alisema
Doku ambaye kwa sasa amerejea mazoezini na klabu yake hiyo so far amefunga mabao mawili pekee na asisti 2 katika mechi 13 alizocheza msimu huu.