Africa

Nabi ataka alama 6 shirikisho Afrika

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema timu yake italazimika kushinda michezo dhidi Real Bamako na US Monastir ili kujiweka mazingira mazuri Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidhi ya Real Bamako Machi 8 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tumejiandaa vizuri na mechi ya kesho na ili tusonge mbele mchezo dhidi ya Bamako na mchezo unaofuata ni muhimu kushinda maana mchezo wa mwisho utakuwa mgumu sana,” amesema Nabi.

Yanga itacheza mechi ya mwisho ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ugenini dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button