Africa

Osimhen: Nigeria lazima ijisahihishe

LAGOS, Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen amesema timu yake hiyo ni lazima isahihishe makosa waliyoyafanya katika mzunguko wa kwanza wa michezo ya kufuzu kombe la dunia la 2026 ikiwa wanataka kufufua matumaini ya the Super Eagles kurejea kwenye Kombe la Dunia mwakani.

Nigeria waliokosa makala iliyopita ya kombe la Dunia nchini Qatar baada ya kupoteza michezo miwili ya playoff dhidi ya Ghana wameanza vibaya kampeni hiyo baada ya kupata sare katika michezo yao mitatu ya awali na sasa watakutana na vinara wa kundi lao timu ya taifa ya Rwanda Ijumaa.

Osimhen ambaye anarejea kikosini baada ya kukosa michezo yote ya awali amemwambia mchezaji wa zamani wa timu hiyo John Obi Mikel kwenye podcast ya ‘Obi one podcast’ kuwa anatumaini wachezaji wenzake watajirekebisha na kufanya vizuri kwenye michezo iliyosalia.

“Ni ndoto ya kila mchezaji kijana kuwa kwenye kombe la dunia mimi nikiwemo, nataka kuwepo kama ambavyo kila mchezaji wa the Super Eagles na tunautazama mchezo dhidi ya Rwanda kama sehemu yetu ya kurekebisha makosa tuliyofanya kwenye michezo iliyopita, tuko tayari” amesema

Kurejea kwa Osimhen kwenye kikosi hicho ni mwanga kwani timu hiyo imekuwa ikipata tabu kupata mabao wamefunga manne pekee na kuruhusu matano. Ukilinganisha na hatua kama hii kwenye kampeni ya michuano iliyopita ambako walikuwa na mabao sita huku Osimhen akichangia mawili kati ya hayo

Related Articles

Back to top button