Mitindo

Mwanamitindo Jasinta Makwabe aanza kuiwazia jamii

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO Mtanzania, Jasinta David Makwabe amesema miaka kadhaa mbele atakuwa na kituo maalum kwa ajili ya kusaidia jamii ya Watanzania wenye uhitaji.

Akizungumza naSpotiLEO Makwabe ambaye pia ni mwigizaji amesema mara kadhaa amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji bila kutangaza.

“Kiukweli naamini lazima nitakuja kuanzisha kituo cha watoto yatima na nimekuwa nikisaidia mara kwa mara bila kuonesha na kwa kuonesha, kwahiyo kusaidia ni kitu ambacho nakipenda,” amesema Makwabe.

Akizungumzia eneo la mitindo, Makwabe amesema changamoto kubwa ni malipo, lakini pia hakuna maonesho ya kutosha ya mavazi, ambayo yatakuwa sababu ya wanamitindo wenigi kuonekana.

“Sasa hivi ukimuliza mtu mwanamitindo gani unamjua unakuta ni walewale wa kila siku, sio kwamba wanamitindo hawapo hapana, ila tu hakuna sehemu inaonesha wanamitindo,” amesema Makwabe.

Amesema wakati mwingine inapotokea kazi changamoto inakua kwenye malipo hali hiyo inafanya vijana wanaotamani kuingia kwenye sekta hiyo kukata tamaa.

Makwabe ameongeza kuwa sekta ya burudani ikiwemo uanamitindo mwamko kwa wazazi katika kuwaruhusu watoto wao bado mdogo hali hiyo inafanya wazazi kutowaruhusu watoto wao.

“Uanamitindo kibongobongo ni uongo labda uende nje kwahiyo unakuta kwanza hatuaminiki, pia hakuna maonesho mengi ambayo yanaweza kukutanisha wanamitindo,” ameongeza Makwabe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button