Muziki
Yammy: Zuchu alinipa faraja wakati wa maisha magumu

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva, Yammy, amesema anamshukuru na kumheshimu sana mwanamuziki mwenzake, Zuchu, kwa jinsi alivyomsimamia na kumpa faraja alipokuwa akipitia kipindi kigumu maishani.
Yammy amesema Zuchu alimtafuta kwa njia ya simu na kufanya naye mazungumzo ya muda mrefu yaliyolenga kumtia moyo, kumfariji na kumpa ushauri wa kujenga.
Kwa mujibu wa Yammy, maneno na ushauri alioupata kutoka kwa Zuchu ulimsaidia kurejea katika hali nzuri ya kisaikolojia na kumjenga upya katika mtazamo chanya wa maisha.
“Ninamuheshimu sana Zuchu kwa sababu alinionyesha upendo wa kweli wakati nilipokuwa nahitaji faraja na mtu wa kunitia moyo,” amesema Yammy.




