Tennis

Frizi atwaa taji la Mubadala DC Open

WASHINGTON DC: Nyota wa tenesi wa Marekani, Taylor Fritz, amerejea kwenye njia yake ya ushindi baada ya kutwaa taji la Mubadala DC Open kwa kumshinda Rafael Jódar raia wa Hispania, kwa seti 7-6(2), 6-4 katika fainali iliyochezwa kwa ushindani mkubwa.

Ushindi huo unampa Fritz taji lake la kwanza la mwaka 2026 na kumaliza kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja bila kunyanyua kombe, baada ya mara kadhaa kukwama kwenye hatua za mwisho za mashindano makubwa.

Fainali hiyo ilianza kwa ushindani mkali huku Jódar, mwenye umri wa miaka 19, akionyesha kiwango cha juu na kumlazimisha Fritz kwenda kwenye tie-break ya seti ya kwanza. Hata hivyo, uzoefu wa Mmarekani huyo ulimsaidia kutawala muda muhimu wa mchezo kabla ya kuvunja huduma ya mpinzani wake mapema katika seti ya pili na kulinda uongozi wake hadi mwisho.

Mbali na kutwaa ubingwa huo, Fritz ameongeza taji la 11 katika maisha yake ya ATP Tour, ushindi unaompa ari mpya kuelekea michuano ya Canadian Open na US Open, ambako anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji watakaowania makombe.

Kwa upande wa Rafael Jódar, licha ya kupoteza fainali, kijana huyo ameendelea kuwavutia wadau wa tenisi duniani kutokana na kiwango alichoonyesha dhidi ya mmoja wa wachezaji bora wa Marekani, jambo linaloashiria anaweza kuwa nyota mkubwa wa mchezo huo katika miaka ijayo

Related Articles

Back to top button