Michezo Mingine

Pasio kuwa meneja wa Team Amani

AFRIKA KUSINI: Mwendesha baiskeli nyota wa Afrika Kusini, Ashleigh Moolman Pasio, ameandika sura mpya katika historia ya baiskeli Afrika baada ya kutangaza kuwa atakuwa Meneja Mkuu wa Team Amani mara baada ya kustaafu mashindano mwishoni mwa msimu wa 2026.

Moolman Pasio akieleza dhamira yake ya kutumia uzoefu wake wa muda mrefu katika mchezo huo kuikuza Team Amani na kuifikisha kwenye jukwaa kubwa la dunia.

Moolman Pasio, ambaye ni miongoni mwa wanamichezo wakubwa wa baiskeli kutoka Afrika, anatarajiwa kusimamia mipango ya timu hiyo inayojumuisha kikosi cha wanawake na wanaume pamoja na programu ya kukuza vipaji.

Lengo kubwa la Team Amani ni kuhakikisha kikosi cha wanawake kinapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kifahari ya Tour de France Femmes ifikapo mwaka 2028, hatua ambayo itakuwa mafanikio makubwa kwa baiskeli ya Afrika Mashariki na bara zima la Afrika.

“Nitajiunga na Team Amani kama Meneja Mkuu nikiwa na lengo moja kubwa; kusaidia kuifikisha timu ya wanawake kwenye mstari wa kuanzia Tour de France Femmes mwaka 2028,” alisema Moolman Pasio.

Team Amani, ambayo ina waendesha baiskeli kutoka Afrika Mashariki, imekuwa ikijenga msingi wa kuwapa nafasi wanamichezo wa Afrika kushindana kwenye ngazi ya kimataifa. Timu hiyo imeweka mkazo katika kukuza vipaji vya ndani badala ya kutegemea uhamisho wa wanamichezo kwenda Ulaya pekee.

Uamuzi wa Moolman Pasio kujiunga na uongozi wa timu hiyo umetajwa kuwa hatua muhimu kwa mustakabali wa baiskeli Afrika, kutokana na uzoefu wake mkubwa wa mashindano ya kimataifa na mafanikio aliyopata akiwa mwanamichezo.

Related Articles

Back to top button