Mitindo

Jasinta Makwabe: Vijana wasome kabla ya kufanya mitindo

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO Jasinta David Makwambe amewashauri vijana wanaotamani kuingia kwenye uanamitindo kusoma kwanza ili kufanikisha ndoto zao wakiwa na elimu.

Makwabe amesema anaamini zaidi kwenye elimu na kwamba vijana kuingia kwenye mitindo wakiwa na elimu itawasaidia kufanya vizuri zaidi.

“Mimi nimefanya vitu vyote hivyo nikiwa shule, nimeanza nikiwa shule, wasiache shule kwa sababu ya kuingia kwenye mitindo, wanaweza kufanya wakiwa wanasoma wakiwa na nafasi ila hiyo ni chuo maana ndo unaweza kufanya ukiwa huru,” amesema Makwabe.

Akizungumzia wanamitindo waliomvutia kuingia kwenye sekta hiyo, Makwabe amewataja Flaviana Matata, Miriam Odemba kuwa ni miongoni mwa wanamitindo waliofanikisha uwepo wake kwenye eneo hilo.

Ametaja wanamitindo wa nje kuwa ni Naomi Campbell, mwanamuziki Rihanna na wengine. Amesema tofauti na uanamitindo ni mfanyabiashara.

Novemba 2023, Jasinta Makwabe aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa ya Future Face 2023 yaliyofanyika Novemba 25 nchini Nigeria.

Related Articles

Back to top button