Nyumbani

UMISETA YAANZA KUTIMUA VUMBI TABORA

Mashindano ya 28 ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yamefuliwa leo mkoani Tabora ambapo tayari mikoa kadhaa imeanza vyema safari ya kuwania ubingwa wa michezo hiyo.

Katika michezo ya awali hatua ya makundi kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana, wenyeji Tabora wameichapa Kigoma pointi 48-24, Dodoma ikilala kwa Mbeya kwa pointi 51-29.

Kwenye mchezo wa mpira wa wavu wasichana Katavi imefungwa na majirani zao Rukwa kwa seti 0-3, Manyara imeichapa Dodoma kwa seti 3-0 wakati kwa upande wa wavulana Dar es Salaam wameichapa Arusha kwa seti 3-0 huku Mara ikiishinda Mtwara kwa seti 2-1.

Katika mchezo wa mpira wa mikono wasichana, Manyara imeishinda Njombe mabao 11-10, Pwani ikilala dhidi ya Kagera kwa mabao 24-12 na Tabora ikiwafunga Kilimanjaro kwa mabao 32-18.

Kundi B Shinyanga ilikuwa hoi kwa Mbeya kwa mabao 23-11 na Dar es Salaam ikiishinda Katavi mabao 18-12 huku kwa kindi C Tanga ikiichapa Mwanza kwa mabao 23-12 na Singida ikiishinda Rukwa mabao 13-12 wakati kundi D Mara ikiishinda Kigoma mabao 22-16 na Iringa ikiishinda Lindi kwa mabao 12-8.

Katika mchezo wa soka wavulana, Unguja imetoka sare na Kilimanjaro na Morogoro ikiibuka kidedea kwa mabao 3-1dhidi ya Iringa.

Pia Singida imeichapa Arusha kwa mabao 2-1, Dodoma ikatoshana nguvu na Mwanza baada ya kutoka sare na Geita ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi Mara na Mtwara ikiwachapa kwa bao 2-0.

Related Articles

Back to top button