Ligi Kuu

Mukwala kufuta rekodi ya Kibadeni Kariakoo Derby?

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Simba, Steven Mukwala, anatajwa kuwa na uwezo wa kufuta rekodi ya Abdallah “King” Kibadeni ya kufunga hat-trick kwenye Kariakoo Derby.

Gwiji wa zamani wa Simba, Kibadeni, ameonesha imani kuwa Mukwala anaweza kufanikisha hilo katika mchezo wa Machi 8 dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya Mukwala kufunga hat-trick katika ushindi wa Simba dhidi ya Coastal Union, Kibadeni anahisi nyota huyo wa Uganda anaweza kufuata nyayo zake na kuweka rekodi mpya katika derby hiyo maarufu.

“Nimeona ana uwezo mkubwa wa kufunga. Kama ataendelea na kiwango kile, basi ana nafasi ya kuifikia au hata kuipita rekodi yangu,” amesema Kibadeni.

Pamoja na hayo, Kibadeni anasisitiza kuwa mchezo wa Kariakoo Derby hauwezi kutabirika.

“Mechi hii ni tofauti, kila timu ina nafasi ya kushinda. Nimeangalia viwango vya Simba na Yanga, zote zina safu imara za ulinzi na ushambuliaji,” ameongeza.

Tangu miaka ya 1970 na 1980, Kibadeni ameendelea kushikilia rekodi ya kipekee ya kuwa mchezaji pekee aliyewahi kufunga hat-trick kwenye Kariakoo Derby.

Related Articles

Back to top button