Ligi KuuNyumbani

Viwanja vinne kivumbi Ligi Kuu

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo minne Dar es Salaam, Mwanza, Kagera na Kigoma.

KMC inayoshika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 18 itakuwa mwenyeji wa Geita Gold iliyopo nafasi 14 ikiwa na pointi 17.

Kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Mtibwa Sugar iliyopo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 9 itakuwa mgeni wa Singida Fountain Gate iliyopo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 21.

Kagera Sugar yenye pointi 22 katika nafasi ya 7 itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania inayoshika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 17.

Huko KIGOMA kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Namungo iliyopo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 17 itakuwa mgeni wa Mashujaa inayoshika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 18.

Related Articles

Back to top button