Mtoko wa Pasaka sasa ni wasanii wote

DAR ES SALAAM: Mwimbaji wa muziki wa injili Christina Shusho amesema Rais Samia Suluhu Hassan amebariki tamasha la mtoko wa Pasaka na hivyo, msimu huu wa tatu litapambwa kwa burudani na maombi kutoka kwa wasanii wa madhehebu yote ya dini nchini.
Katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Shusho ambaye ndiye mwanzilishi wa tamasha hilo amesema tamasha hilo litakalofanyika April 20, mwaka huu litakuwa bure msimu huu tofauti na miaka mingine limekuwa ni kwa kiingilio.
Amesema kwa kuwa mwaka huu ni uchaguzi wanataka kutumia tamasha hilo kuimba,kusifu na kuliombea Taifa.
“Sisi ni wananchi wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania tunahusika sana kuliombea Taifa letu. Mwaka huu mtoko hautakuwa kama ilivyokuwa miaka ya ya nyuma bali ni waimbaji wote wa nyimbo za injili,
Amesema:”Kiukweli tumepewa nguvu na Rais Samia Suluhu Hassan , tunamshukuru mama kwa kutambua muziki huu, anaamini nyimbo zetu zinaweza kufanya jambo katika uchaguzi wa mwaka huu,”
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria ni John Kavishe aliyesema anamshukuru Christina Shusho, serikali kuona Kuna nafasi ambayo wanamuziki wa injili wanaweza kufanya kitu.
“Ni upumbavu au mtu asiyekuwa na hekima kushindwa kukusanyika kwasababu ya udini. Tuko tayari tumejiandaa itakuwa ni kitu ambacho hakijawahi kutokea,”amesema.
Naye Japhet Zabroni amemshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka wasanii wa muziki wa injili na kuahidi watafanya vizuri.