Muziki

Diamond Platnumz: Wimbo wa ‘Komasava’ niliuombea

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameweka wazi wimbo wake unaofanya vizuri wa ‘Komasava’ kwamba aliuandaa kipindi cha mfungo wa Ramadhani ndiyo maana unapata mafanikio makubwa.
“Niliandika wimbo huo Ramadhani ya 27, nilikuwa pale na mtayarishaji wangu, tukirekodi, na ulikuwa wakati wa kwenda kwa ajili ya swala ya Tahajjud.

Mazingira ya siku hiyo ni maalum sana kwa Waislamu; unapoomba, Mungu hutimiza matakwa yako. Kwa hiyo, niliomba kisha nikarudi studio kuendelea kurekodi.”

Diamond aliendelea kuuelezea wimbo huo kuwa “Tulipokuwa tunarekodi wimbo huo, tulilenga kuunda kitu kitakachodumu wimbo unaounganisha watu. Ndiyo maana nilijumuisha lugha nyingi kama vile Kifaransa, Kiswahili, Kilatini, na Kizulu.

Wimbo huo unaelezwa kwamba aina yake ya uchezaji ulitungwa kwa lengo la kujumuisha watu wote katika furaha.

Tangu wimbo huo ulipoachiwa Mei 3, 2024, umeangaliwa na zaidia ya watu milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube, zaidi ya milioni 5 kwenye Boomplay, na zaidi ya milioni 2.6 kwenye Spotify.

Related Articles

Back to top button