Nyumbani

Mshindi wa Muhalila cup kujipatia milioni 2

KAGERA: Timu 16 kutoka kata mbalimbali Wilaya ya Muleba zimeanza kuachuana katika ligi ya Muhalila Cup ambayo hufanyika kila Novemba mpaka Desemba mkoani Kagera kwa lengo la kukaribisha wageni wanaoishi mikoa ya nje ,na nje ya Tanzania Kama sehemu ya burudani wanaporudi nyumbani kusherekea sikukuu.

Mkurugenzi wa mashindano hayo, Fortunatus Muhalila amesema kuwa hii ni mara ya tisa mfululizo mashindano hayo yanafanyika ambapo kwa mwaka huu licha ya kukaribisha wageni bado kuna Elimu ya utunzaji wa mazingira na upambanaji wa uvuvi haramu kutokana na wilaya hiyo kuwa na visiwa vingi huku vijana wengi wakiwa miongoni mwa wavuvi wasiofuata sheria za uvuvi.

Amesema kuwa ligi hiyo itazikutanisha timu 16 na fainali zinatarajia kufanyika Desemba 31 huku mshindi wa kwanza akijipatia jezi,mpira,kikombe na fedha taslimu Sh milioni mbili,mshindi wa pili atapata jezi mpira na Sh milioni moja huku mshindi wa tatu akipata kiasi cha Sh laki tano.

Katika ufunguzi wa ligi hiyo ,timu ya, New Muleba Breaking News ilijipatia  ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Muyenje huku muandaaji wa mashindano hayo akijivunia kuibua vipaji tangu ligi hiyo ilivyoanzishwa mwaka 2015 na kudai kuwa baadhi ya vijana waliopitia ligi hiyo wanacheza katika vilabu mbalimbali vya ligi daraja la kwanza na ligi kuu Tanzania.

Ufunguzi wa mashindano hayo pia umetoa Fursa kwa shule 19 za sekondari kupata  vifaa vya michezo mbalimbali.

Mdau wa michezo nchini, Shafii Dauda ambaye alihudhuria ufunguzi wa ligi hiyo alisema kuwa ni vizuri vijana ambao wanashiriki katika ligi mbalimbali  za ndondo kuhakikisha wanania na malengo ya kile wanachokipigania kwa sababu mpira unachangamoto kubwa kabla ya mafanikio.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Abel Nyamahanga alisema kuwa  serikali kwa kushirikiana na wadau wamichezo  wataboresha Uwanja wa Kagoma ambao unatumika katika mashindano hayo ili vijana wacheze vizuri zaidi na kuonyesha vipaji vyao huku akiwataka kudumisha mshikamano na amani katika mashindano hayo.

 

Related Articles

Back to top button