BAADA ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam leo inashuka tena dimbani ugenini kuikabili Ihefu.
Mchezo huo pekee wa ligi hiyo leo utafanyika kwenye uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali, mkoani Mbeya.
Katika mchezo uliopita wa ligi, Ihefu imetoka sare ya mabao 2-2 na Singida Fountain Gate kwenye uwanja wa Liti mjini Singida.