Afrika MagharibiAfrika Mashariki

Mgunda: Stars bado hatujamaliza kazi

KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars Juma Mgunda amesema kazi bado haijasha Stars hivyo, hawapaswi kubweteka zaidi ni kujipanga na michezo miwili ijayo dhidi ya DR Congo.

Mgunda amesema hayo baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea jana nchini Ivory Coast huku akiweka msisitizo kuwa bado wapo kwenye marathon wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika michezo ijayo.

Amesema: “Tunawashukuru vijana kwa kujituma na kuonesha juhudi lakini nieleze kuwa hii ni marathon tuna kazi kubwa mbele, tutapumzika kidogo kisha tutarudi kujiandaa na michezo miwili ijayo,”.

Stars imefika pointi nne nyuma ya kinara DR Congo mwenye pointi sita katika kundi H kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Afrika za Morocco za 2025.

Mchezo ujao dhidi ya DR Congo kuhitimisha mzunguko wa kwanza utachezwa Oktoba 7, mwaka huu ugenini na kurudiana Dar es Salaam Oktoba 15 katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kundi hilo.

Kwa mujibu wa Mgunda, kwa sasa ni mapema mno kuona kama wamefuzu wanatakiwa wapambane mpaka mwisho kujua hatma yao ya kusonga mbele.

Kuhusu mchezo huo uliopita, amesema vijana wamecheza kwa maelekezo na mwisho wa siku wakapata matokeo ambayo yamewapa matumaini mapya ya kufanya vizuri zaidi katika michezo ijayo.

 

Related Articles

Back to top button