Afrika Mashariki

Maandamano ya Kenya yaahirisha wimbo wa Tanasha

NAIROBI, Kenya: MPENZI wazamani wa msanii Diamond Platnumz, Tanasha Donna ametangaza kuahirisha kuachia wimbo wake mpya siku ya Ijumaa kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Kenya ya maandamano wanaopinga Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024.

Tanasha ameandika katika ukurasa wake wa Instagram, kwamba alishaandaa kila kitu kwa ajili ya kuachia wimbo wake mpya siku ya Ijumaa, lakini amelazimika kusitisha mchakato huo ili kuomboleza waliopoteza maisha kwenye maandamano hayo.

Tanasha ambaye ni mama wa mtoto mmoja amesema kwa sasa hana uhakika ni siku atakayouachia wimbo huo mpya hadi hali ya maandamano itakapoisha.

“Singo yangu ya kwanza kutoka katika kazi zangu mpya ilipaswa kutolewa leo, lakini tunaomboleza vifo vya mashujaa wetu wachanga hadi machafuko yatakapokamilika ndiyo nitauachia,” Donna ameandika.

Machafuko yameshuhudiwa nchini humo hasa jijini Nairobi na vitongoji vyake kwa muda wa wiki mbili zilizopita baada ya vijana wa Gen Z kutangaza ‘punda amechoka’ na kujitokeza kwa wingi kuandamana wakitaka kufutwa kwa mswada huo wenye utata.

Hata hivyo, siku ya Ijumaa, Mahakama Kuu iliamuru kwamba polisi wasitumie nguvu kupita kiasi kuwatawanya waandamanaji, ikiwa ni pamoja na kutumia vitoa machozi, maji ya kuwasha au risasi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button