Ligi Daraja La Kwanza

Mexico yaweka rekodi mpya tangu Italia 1990

MEXICO:TIMU ya taifa ya Mexico inaendelea kuwa gumzo kubwa kwenye Kombe la Dunia 2026 kutokana na rekodi na kiwango kikubwa ilichokionesha tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Mexico sasa imefikisha mechi 10 za Kombe la Dunia katika Uwanja wa Azteca bila kupoteza hata moja, jambo linaloendelea kuifanya Azteca kuwa moja ya ngome ngumu zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Katika Kombe la Dunia la mwaka huu, Mexico imecheza mechi nne na kushinda zote nne, ikifunga mabao nane huku ikitunza ‘clean sheet’ katika kila mchezo.

Kwa mafanikio hayo, Mexico imekuwa timu ya kwanza tangu Italia mwaka 1990 kuanza Kombe la Dunia kwa ushindi wa mechi nne zote huku ikimaliza kila mchezo bila kuruhusu bao.

Safu yao ya ulinzi imekuwa moja ya siri kubwa za mafanikio hayo, kwani katika mechi nne walizocheza wamekabiliwa na mashuti sita tu yaliyolenga lango, takwimu zinazoonesha uimara mkubwa wa mfumo wao wa kujilinda.

Mbali na rekodi za timu, Mexico pia imepata nyota mpya wa kuvutia katika mashindano haya. Gilberto Mora mwenye miaka 17 na siku 259 ambaye ameweka historia kwa kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuanza mechi ya hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, akitanguliwa na Pelé aliyefanya hivyo mwaka 1958.

Kwa kiwango walichokionesha hadi sasa, Mexico inaonekana kuwa moja ya timu zinazoweza kusumbua vigogo wengi katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia 2026.

Related Articles

Back to top button