Nyumbani
Maudhui yazingatie Utamaduni wa Kitanzania-Gekul

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amewataka waandaaji na wazalishaji wa maudhui kuzingatia mila na desturi za Tanzania.
Gekul ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa Sekta ya Utangazaji Tanzania.
Amesema kuwa ni jukumu la wadau hao wa utangazaji kuchuja maudhui kabla ya kuyafikisha kwa jamii ili yasilete athari za kudidimiza utamaduni wa Taifa.
“Vyombo vyenu visiwe chanzo cha kubomoa utamaduni wetu.Tuandae maudhui ambayo yatasaidia kulinda mila na desturi zetu,” amesema Gekul.
Aidha, amewataka wadau hao kutumia nafasi zao katika kukuza maudhui ya ndani ikiwemo sanaa, filamu, muziki, sanaa za maonesho zinazozalishwa ndani ya jamii husika.