Nyumbani

Azam FC kucheza mechi ya kirafiki na JKT kujiandaa na Kengold

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Azam FC kipo kwenye maandalizi kabambe kuelekea kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo kesho, Alhamisi, Machi 27, kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka’, timu hiyo imekuwa ikitumia kipindi hiki cha mapumziko kwa kucheza mechi tatu za kirafiki kama sehemu ya maandalizi. Tayari wamecheza michezo miwili, na mchezo wa kesho utakuwa wa mwisho kabla ya kurejea kwenye ligi.

“Kipindi hiki ligi imesimama, hivyo tulipanga kucheza mechi tatu za kirafiki. Tumeshacheza mbili, na mchezo wa mwisho Alhamisi ni maandalizi kuelekea mchezo wetu wa ligi dhidi ya Kengold FC,” amesema Zaka.

Ameongeza kuwa wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu ya taifa wanaendelea vizuri na maandalizi, huku benchi la ufundi likihakikisha kikosi kinakuwa katika hali bora.

Azam FC inatarajia kusafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Kengold FC, utakaopigwa Aprili 3 kwenye Uwanja wa Sokoni, Mbeya.

Mechi hiyo ni muhimu kwa Azam FC katika harakati zao za kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

Related Articles

Back to top button