Nyumbani

Mashujaa FC waitamani CHAN

DAR ES SALAAM: KLABU ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma imepiga hodi Bodi ya Ligi kuu Tanzania kuomba msaada wa kupata timu zitakazokuja nchini kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa ajili ya mechi za kirafiki.

Meneja wa timu hiyo, Athumani Amiri amesema kipindi Ligi imesimama wachezaji wamepewa mapumziko na kurejea kambini Januari 13, wataingia kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa na Ligi inayotarajia kurejea Machi Mosi mwaka huu.

“Ripoti ya Kocha Abdallah Mohammed ‘Bares’ imehitaji timu kupata mechi za ushindani za kirafiki katika kipindi tutakachokuwepo kambini, tumefanyia kazi na kupeleka maombi Bodi ya Ligi Tanzania kuweza kutusaidia kupata timu zinazotoka nje zinazokuja kucheza michuano ya CHAN,” amesema.

Athumani amesema anaimani wakipata mechi za kirafiki kadhaa kutoka katika timu hizo kutawasaidia kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya NBC.

Related Articles

Back to top button