Muziki

Marioo asalimu amri Basata

Msanii wa Bongo fleva, Omary Mwanga, ‘Marioo’ leo ameitikia wito na kufika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhusu sakata la wimbo wake wa ‘Iphone users’ alioutoa hivi karibuni kuwa na maneno yaliyoleta utata katika jamii.

Marioo amefanya majadiliano na Katibu Mtendaji wa BASATA Dk. Kedmon Mapana kuhusiana na sakata la wimbo wake wa ‘Iphone users’ alioutoa Msanii huyo kuwa na maneno yaliyoleta utata.

Katika kikao hicho Dk. Mapana ametumia fursa hiyo kuwataka Wasanii wazingatie na kuusoma Mwongozo wa maadili katika kazi za Sanaa ambao ulitolewa na Baraza hilo, mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya BASATA, wanapaswa kupitia.

Aidha Katibu Mtendaji pia alimkabidhi Mwongozo wa Baraza hilo Msanii Marioo aliyeitwa barazani hapo kwa lengo la kuonywa.

Pia Marioo ametakiwa akafanye marekebisho katika nyimbo yake ya ‘Iphone user’ na kuondoa maneno ambayo yanaelezwa kuwa na utata kwenye jamii.

Baraza limekuwa likiwaita mara kwa mara wasanii na kuwarekebisha pindi wanapoenda kinyume na taratibu bila kufanya Mila na Desturi za Tanzania

Related Articles

Back to top button