Muziki

Diamond ashinda tuzo Nigeria

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameshinda tuzo ya Msanii Bora wa Kimataifa wa Afrika katika tuzo za Galaxy Music Awards zilizotolewa jana nchini Nigeria.

Diamond alishindana na mastaa wengine wa Afrika, akiwemo Black Sherif wa Ghana, Tyla Laura ‘Tyla’ wa Afrika Kusini, Divine Ikubor ‘Rema’ wa Nigeria, Kelvin Momowa wa Afrika Kusini, Livingstone Satekla ‘Stonebwoy’ wa Ghana, na Fally Ipupa wa DR Congo.

Mbali na kushinda tuzo hiyo, Diamond anaendelea kuthibitisha umaarufu wake kama mmoja wa wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki. Takwimu kutoka Charts Tanzania zinaonesha kuwa msanii huyo ameweka rekodi kwa kufikisha jumla ya streams 500,000,000 kwenye mtandao wa kusikiliza muziki wa Boomplay, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kufikiwa na msanii yeyote wa Afrika Mashariki.

Hii ni ishara kuwa muziki wake unaendelea kupendwa na kufuatiliwa na mashabiki wengi barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button