Mariah Carey kufanya ziara ya Krismasi kwa miji 20 Marekani

NEW YORK: MALKIA wa nyimbo za Krismasi, Mariah Carey atatembelea miji 20 ndani ya Marekani katika kuadhimisha miaka 30 ya albamu yake ya Krismasi njema na ‘All I Want for Christmas Is You’.
Mariah Carey mwenye rekodi zaidi ya milioni 200 zilizouzwa duniani kote ametangaza kwamba tamasha lake la kila mwaka la Krismasi limerejea na kwa sasa amelifanya kuwa la kitaifa!
Wakati wa Krismasi Mariah Carey ametangaza kutembelea miji 20 kote nchini Marekani na ziara hiyo itaanza Novemba 6 ambapo ataanza na Jiji la Los Angeles, Houston, Atlanta, Philadelphia na zaidi kabla ya kumalizia ziara yake Desemba 17 katika mji wake wa NYC.
Ziara hiyo imetayarishwa na Live Nation. Mariah Carey atatumia ziara hiyo kusherehekea kumbukumbu ya miaka 30 ya albamu yake ya nyimbo za Chrismas ya ‘Merry Christmas’ pamoja na wimbo wake uliovunja rekodi wa ‘All I Want for Christmas is you’.
Kumbi zitakazotumika katika maonesho hayo ni pamoja na Yaamava Theater, Acrisure Arena, Moody Center, Toyota Center, Airlines Center, State Farm Arena, Bridgestone Arena, Allstate Arena na Enterprise Center.
Kumbi nyingine ni Capital One Arena, Wells Fargo Center, TD Garden, CFG Bank Arena, PNC Arena, PPG Paints Arena, Prudential Center, UBS Arena na Barclays Center.