Muziki
Rais Samia amzawadia milioni 50 mtunzi mkongwe wa wimbo wa Tanzania

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amemzawadia kiasi cha Shilingi milioni 50 mwimbaji wa muziki wa zamani mzee Steve Hiza aliyeimba wimbo wa ‘Tanzania ndiyo nchi ya Furaha’.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa Hafla ya Tuzo za Muziki Tanzania ( TMA ) ambapo amesema Mhe Rais ametoa zawadi hiyo Mahususi kwa Mzee Hiza kutokana na mchango wake kwenye Muziki.
“Tanzania yetu ndio nchi ya furaha, kote ulimwenguni watu wote wanajua…” ni moja ya kionjo cha wimbo huo mkongwe ambao ni maarufu midomoni mwa watu kwa kuwa mara nyingi umeimbwa na Mzee Stephen Hiza.