EPL
Maresca awachana makavu mabeki wake

LONDON: Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca ameonesha kukerwa na safu ya ulinzi ya klabu hiyo baada ya kuonekana ikipitika kirahisi na wapinzani wao akisema safu hiyo inapaswa kupambana sawa na ile ya ushambulizi ili timu hiyo iwe salama kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Kauli ya Maresca inakuja baada ya Chelsea kuruhusu bao 3 katika mchezo wao wa wikiendi iliyopita dhidi ya Tottenham Hotspur wakishinda bao 4 kwa 3 lakini safu hiyo imekuwa ikiruhusu golikipa wao Robert Sanchez kufikiwa mara kwa mara.
“Hutashinda mechi au vikombe kwa kufunga magoli tu, unahitaji kulinda. Hata baada ya kuruhusu bao 3 dhidi ya Spurs hatuko vibaya, kuna wanaofungwa zaidi yetu lakini hii haitufanyi tuache kujiimarisha hasa kiulinzi. Nadhani watu wa eneo hilo wanajua cha kufanya” Maresca amewaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa Europa league dhidi ya Astana
Chelsea walio nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu ya England wakiwa na points 31, wameruhusu mabao 18 katika mechi 15.