EPL

Man United yarudi mlangoni mwa Ligi ya Mabingwa, maamuzi mazito yaja

LONDON:KLABU ya Manchester United ipo hatua moja tu kurejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford, lakini pamoja na mafanikio hayo, uongozi unakabiliwa na maamuzi magumu kuelekea msimu ujao.

Kiungo mkongwe Carlos Casemiro, mwenye umri wa miaka 34, aliendelea kuwa mhimili wa timu hiyo baada ya kufunga katika mechi ya tatu mfululizo nyumbani.

Hata hivyo, kocha Michael Carrick amethibitisha kuwa kiungo huyo anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu, hali inayolazimisha klabu hiyo kuanza harakati za kuziba pengo lake.

Carrick amesema mchango wa Casemiro hauwezi kupuuzwa, lakini ni kawaida kwa wachezaji kuondoka na wengine kuingia.

Kuondoka kwake kunafanya eneo la kiungo kuwa kipaumbele kikubwa kwa mabosi wa Old Trafford.

Katika mipango ya usajili, United inalenga kusajili viungo wawili au watatu, huku jina la Elliott Anderson likitajwa kuwa chaguo la kwanza. Hata hivyo, klabu hiyo imeweka msimamo mpya wa kutotumia fedha nyingi kupita kiasi na kuepuka mikataba mikubwa inayoweza kuwa mzigo baadaye.

Mbali na usajili, mustakabali wa Carrick nao bado haujawa wazi. Wapo wanaoamini kuwa ameifanya kazi kubwa ya kuipeleka timu karibu na Ligi ya Mabingwa hivyo anastahili kupewa mkataba wa kudumu. Lakini wengine wanaona klabu inapaswa kutafuta kocha mwenye uzoefu zaidi.

Majina ya makocha kama Luis Enrique na Julian Nagelsmann yametajwa, lakini uwezekano wa kuwapata unaonekana kuwa mdogo kutokana na mikataba yao na gharama kubwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button