EPLKwingineko
Pochettino akodolea macho ukocha Chelsea
Mauricio Pochettino anakodolea macho sakata linaloendelea Chelsea ‘The Blues’ huku shinikizo likiendelea kupanda kwa dhidi ya Graham Potter.

Potter, kocha wa zamani wa Brighton alichukua mikoba Stamford Bridge Septemba, 2022 tu, lakini kwa sasa The Blues inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu England(EPL) na tayari imeondoshwa katika michuano ya ndani.
Pochettino hana timu tangu alipotimuliwa Paris Saint-Germain (PSG) msimu uliopita lakini atakuwa tayari kuchukua mikoba Chelsea iwapo Potter atatimuliwa.
Ripoti zimesema tayari Bodi ya Chelsea inafikiria hatma ya Potter na huenda akatimuliwa Januari 12 iwapo Chelsea itafungwa katika mchezo wa EPL ugenini dhidi ya Fulham.




