Muziki

Akothee arudisha mpira kwa kipa, kurudi uwanjani 2027

NAIROBI: KUPITIA kazi yake ya muziki, mama huyo wa watoto watano amejijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Kenya na sasa ni mmiliki wa kampuni ya usafirishaji huku akiendelea kuwa balozi wa kampuni mbalimbali.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Akothee alikiri kutojihusisha na muziki kwa muda mrefu lakini pia amedai hakuacha bali kwa kuwa ameanzisha kampuni ya usafirishaji hivyo muda mwingi ameutumia kwenye kazi hiyo mpya.

“Kwa wale wanaojiuliza ikiwa nimeacha kuimba: kila kitu kina wakati wake. Unajenga taaluma yako kwanza, kisha tumia taaluma hiyo kuimarisha uwezo wako mwingine,” alisema Akothee.

Akothee alitaja kuwa kwa sasa yuko shuleni akijifunza kuhusu maendeleo ya kibinafsi na atarejea kwenye ulingo wa muziki kwa nguvu zote baada ya miaka mitatu yaani hadi mwaka 2027.

“Kwa sasa, nimerejea shuleni kwa ajili ya ukuaji wangu binafsi, lakini nitarejea kwenye muziki 2027. Kwa sasa, jiandikishe kwa chaneli yangu ya YouTube. Hasa albamu yangu ya ‘Sibuor Madhako’,” alisema.

Related Articles

Back to top button