Ashanti, Nelly wamuweka wazi mtoto wao wa kiume

NEW YORK:WANAMUZIKI Ashanti Douglas mwenye miaka 43 na Cornell Haynes maarufu Nelly mwenye miaka 49 wamemuweka wazi mtoto wao Kareem Haynes katika mitandao ya kijamii baada ya mwezi mmoja kupita tangu alipozaliwa Julai 18 mwaka 2024.
Wawili hao walifunga ndoa mnamo Desemba 2023 na baada ya kupata mtoto huyo walifanya siri hadi jana Agosti 21, Ashanti alipoamua kuweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii akionyesha mwili wake tangu alipojifungua mwezi mmoja uliopita.
Mwakilishi wa wanandoa hao aliiambia People: “Ashanti na Nelly walikuwa na furaha mno walipomkaribisha mtoto wao wa kiume, Kareem,”
Ashanti aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akionyesha mwili wake mwezi mmoja baada ya kujifungua.
Alisema: “Wiki nne baada ya kujifungua. Hujui mwili huu unaweza kufanya nini!”
Katika maelezo ya chapisho hilo, Ashanti alibainisha Siku zote haiko kwa wakati, hakuna kitu ambacho kingeweza kumwandaa kuwa mama, bila kujali ni miaka mingapi alikuwa akiitamani.
Alisema: “Inachekesha jinsi mipango ya maisha. Nimekuwa nikingojea kuwa mama kwa muda mrefu sasa lakini hakuna kitu kinachoweza kunitayarisha kwa kila kitu kinacholetwa na mama! Hivi ndivyo inavyoonekana baada ya kuzaa napenda kaptura hizi za kupendeza.,Ninajivunia mwili wangu kwa kunipa mtoto wangu, mtoto, mtoto, mtoto, mtoto,”.
Nelly tayari ana binti anayeitwa Chanelle mwenye miaka 30 na Cornell mwenye miaka 25 aliyezaa na mke wake wa zamani Channetta Valentine. Nelly pia alimchukua mpwa wake Shawn mwenye miaka 27 na mpwa wake Sydney mwenye miaka 20, kufuatia kifo cha mama yao mnamo 2005.
Ashanti na Nelly walikuwa katika uhusiano toka 2003 hadi 2013 lakini wakarudiana tena baada ya muongo mmoja baadaye. Ashanti alionekana mwenye furaha mno alipojigundua kuwa alikuwa na ujauzito wa Nelly baada ya kuutafuta kwa muda mrefu.