Kwingineko

Mama Beyonce, aeleza alivyogunduliwa kuwa na saratani

NEW YORK: MAMA wa Beyonce na Solange Knowles, Tina Knowles mwenye miaka 71 ameweka wazi namna alivyopigwa na butwaa wakati madaktari walipogundua saratani ya matiti ya hatua ya 1 kwenye titi lake la kushoto mwaka jana.

Mama huyo anasema awali alikosa kipimo cha kawaida cha ‘mammogram’ na tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya yeye na Beyonce, kuzindua laini yao ya huduma ya nywele ya Cecred.

Mama huyo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo na kupunguzwa matiti kwa wakati mmoja na sasa anaendelea vizuri. Na sasa ameamua kuweka wazi jambo hilo kupitia kitabu.

Amesema: “Ninafanya vyema. Bila saratani na nimebarikiwa sana kwamba Mungu aliniruhusu kuigundua mapema. Nina afya bora, ninakula vizuri na nilipunguza uzito.”

Tina anakuwa mwanamke mwenye msukumo kwa wanawake wengine kwa kuwatia moyo wa kujichunguza mapema kuhusu saratani na pia wanapogundua kuwa nayo wawahi matibabu.

Amesema: “Sikujua kwamba kulikuwa na hatua ya awali. Ningeweza kupata hii katika hatua ya 0 ikiwa singekosa mammogram yangu.
“Nataka kuwaonyesha watu kuwa unaweza kupitia hilo na bado uwe salama. Nataka kuwapa watu matumaini. Kinachoniogopesha sasa ni kutotumia vyema kila niliyoacha katika maisha haya.”

Amesema: “Ningetatizika iwapo ningeshiriki safari hiyo katika kitabu kwa sababu mimi ni mtu wa faragha sana. Lakini niliamua kuishiriki kwa sababu nadhani ina mafunzo mengi mno ndani yake kwa wanawake wengine.

“Na nadhani kama wanawake, wakati mwingine tunakuwa na shughuli nyingi na tunajifunga na kukimbia, lakini lazima uende kufanya uchunguzi na kuchukua majibu yake maana kama nisingegundua mapema nini kingenikuta.”

Katika kitabu hicho, Tina ameeleza kwa undani jinsi mabinti zake walichukua habari hiyo.
Amesema: “Beyonce aliikubali vizuri, akiwa na mtazamo chanya, na tayari nilihisi akili yake ikienda mbio na Solange alisema ‘Mama, tutashughulikia hili.”

Related Articles

Back to top button