Kwingineko

Kanu, Nani washiriki miaka 80 ya klabu Ethiopia

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno na Manchester United, Luis Nani na mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu wameanza kazi iliyowapeleka Addis Ababa baada ya kuwasili jana katika mji huo nchini Ethiopia.

Wachezaji hao mashuhuri wanashiriki maadhimisho ya miaka 80 ya kuanzishwa kwa Klabu ya kusaidia na kukuza sekta ya michezo nchini humo Mechal Sports Club, kama wageni wa heshima.

Awali wageni hao walipokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole na Waziri wa Nchi wa Utalii Sileshi Girma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mechal Sports Club, Seife Getahun na Mkurugenzi wa Operesheni za Vyombo vya Habari vya Ulinzi, Brigedia Jenerali Kuma Mideksa.

Klabu ya Mechal ilianzishwa mwaka1936, imekuwa ikishiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za michezo na kuitangaza nchi kupitia viwanja vya michezo vya kimataifa inavyojenga.

Mbali na kuongeza ari ya jeshi katika Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia (ENDF), klabu hiyo pia ilifanya shughuli nyingi kwa ajili ya ustawi wa nchi ikikuza uzalendo kwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.

Mechal Sport Club pia imeleta wachezaji wengi maarufu waliochaguliwa kwenye timu ya taifa ya Ethiopia ambao wamecheza mechi mbalimbali za kimataifa.

Related Articles

Back to top button