EPL

Majeraha yazidi kupiga hodi OT

MANCHESTER: Klabu ya Manchester United imethibitisha kiungo wake wa kati wa Kobbie Mainoo atakuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kupata jeraha la misuli dimbani Villa Park katika mchezo dhidi ya Aston Villa mapema mwezi huu.

Mainoo alikosa mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya wakati timu yake ya taifa ya England ikicheza dhidi ya Ugiriki na Finland kutokana na jeraha hilo, pamoja na mchezaji mwenzake Harry Maguire, ambaye pia hachezi baada ya kupata jeraha katika mchezo huo huo ambao Man United iliambulia sare ya 0-0 dhidi ya Aston Villa.

Klabu hiyo pia imesema washambuliaji wake Alejandro Garnacho, Amad Diallo Beki Noussair Mazraoui, ambao pia walikosa mechi za kimataifa mwezi huu kutokana na majeraha na ugonjwa, wamerejea mazoezini kuelekea mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Brentford.

Majeraha pia yamewaweka nje Luke Shaw, Tyrell Malacia, Mason Mount na Leny Yoro, na hivyo kuongeza ugumu wa United wanaoshikilia nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi nane katika mechi saba.

Related Articles

Back to top button