EPLKwingineko
Arteta: Mechi haitaamua ubingwa EPL
KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta amesema mchezo dhidi ya Manchester City Aprili 26 hautaamua ubingwa wa Ligi Kuu England(EPL).
Vinara wa EPL Arsenal inaoongoza kwa pointi tano ikiwa na pointi 75 mbele ya kikosi cha Pep Guardiola ambacho kina michezo miwili mkononi chenye pointi 70 kabla ya mchezo huo kwenye uwanja wa Etihad.
“Tulijua tunapaswa kwenda Etihad, itakuwa mechi ngumu, lakini je itaamua msimu? Hapana. Tukishinda kesho hatujashinda ligi. Labda itabadilisha asilimia, lakini mechi tano kwenye ligi hii bado ni mtego, “amesema Arteta.
Kwa mara ya mwisho Arsenal ilitwaa taji la EPL mwaka 2004.




