De Bruyne ana mashaka na Haaland

MANCHESTER:KIUNGO mshambuliaji wa Manchester City Kevin De Bruyne amesema hana uhakika kama mshambuliaji wa timu hiyo Erling Haaland anaweza kuwa mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya kandanda ya England licha ya kuongeza mkataba wa kusalia klabuni hapo kwa miaka 9 zaidi.
De Bruyne ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa Sky Sports aliyetaka kujua maoni ya kiungo huyo iwapo kuongeza mkataba kwa Haaland na kasi yake ya kufunga anaweza kumfikia Alan Shearer mwenye magoli 260
“Kwakweli sijui ni magoli 260 na yeye ana 80 mapaka sasa bado ana kazi ya kufunga mabao 181. Kwakweli inabidi akae kwa muda huo (miaka 9 ya mkataba) lakini pia lazima upige hesabu za umri, majeruhi ambayo yanaweza kutokea mda wowote. Lakini akikaa kwa miaka 10 nadhani ana nafasi nzuri, amefunga sana tayari” amesema Kevin De Bruyne
Orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu ya England inaongozwa na Mwingereza Alan Shearer mwenye mabao 260 huku Erling Haaland akiwa katika nafasi ya 21 kwenye orodha hiyo.