Michezo Mingine

Simba vs Yanga Ngao ya jamii wanawake leo

NUSU fainali za michezo ya Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu ya mpira wa wanawake Tanzania Bara zinapigwa leo, Dar es Salaam.

Timu zitakazocheza nusu fainali hizo ni JKT Queens, Yanga, Simba na Fountain Gate Princess.

Nusu fainali ya pili ndio inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa kabumbu kwani itawakutanisha watani wa jadi, Simba Queens dhidi ya Yanga Princess kwenye uwanja wa Azam Complex.

Katika nusu fainali ya kwanza bingwa mtetezi Ligi Kuu bara JKT Queens itakabiliana na Fountain Gate Princess kwenye uwanja huo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button