Filamu

Lupita huyooo kwenye ‘The Wild Robot’

NEW YORK: STAR anayefanya vizuri katika filamu duniani, Lupita Nyong’o wakati huu ataonekana katika filamu ya roboti inayoitwa Roboti Pori ‘The Wild Robot”, ambayo hadithi yake imetoka katika riwaya ya Peter Brown.

Muigizaji huyo mwenye miaka 41 ambaye amefanya vizuri katika filamu ya ‘A Quiet Place: Day One’ iliyotoka mwaka huu wa 2024 ameonyesha kufurahia mradi huo wa filamu ya roboti.

“Oh, Mungu wangu. Yaani nampenda Roz na ninapenda mradi huu,

“Ni jambo zuri Peter Brown ameandika vitabu vitatu! Moyoni nimemtembelea.”

Mkurugenzi Chris Sanders alisifia namna waigizaji walivyojitoa katika filamu hiyo: “Wafanyakazi wote walijihusisha sana kwenye filamu hii kwa njia ambayo sijawahi kuona hapo awali, mimi mwenyewe nikiwemo. Hii ilikuwa kazi ya upendo kwa kila mtu tulipokuwa studio, ningependa kuwa nao kwa muda wote,”

Filamu hiyo ya ‘The Wild Robot’ tofauti na Lupita Nyon’go imeshirikisha waigizaji wengine akiwemo Mark Hamill, Pedro Pascal, Bill Nighy na Catherine O’Hara na itaanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema 18 Oktoba mwaka huu 2024.

Filamu hiyo inaelezea Roz anayekuja kujifunza jinsi ya kukabiliana na kuwasiliana na wanyamapori wa ndani baada ya kuishi kisiwani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button