KONA YA FILAMU

Coming to America, 1988 ‧ Comedy/Romance
LEO tunarudi miaka ya 80 tukiangazia filamu hii ya kuchekesha na iliyojaa mafunzo ndani yake.
Filamu hii ilitoka Mwaka 1988 huko nchini Marekani na kuongozwa na na John Landis. Hadithi ya filamu hii ilitungwa na Msanii maarufu Eddie Murphy ambaye pia aliyeigiza kama muhusika mkuu (Akeem Joffer).
Filamu hiyo pia ameigiza pamoja na Arsenio Hall, James Earl Jones, John Amos, Madge Sinclair, na Shari Headley.
Katika Filamu hii Eddie Murphy anaigiza kama mtoto wa Mfalme katika nchi ya kubuniwa kutoka Afrika ikijulikana kama Zamunda.
Filamu hii ilelenga kuonesha familia ya kitajiri na ya kifalme kutoka Afrika ikiwa na maudhui ya akisalia.
Licha ya malezi ya kifalme Akeem anatarajiwa kufunga ndoa kwa kufuata mila na desturi za kutoka taifa lake ambapo katika siku ya kusherekea sikukuu yake ya kuzaliwa anatakiwa kutafutiwa mke asiyemjua na wazazi wake kutoka familia ya kitajiri ili kuendana na hadhi ya familia yake.
Mambo yanabadilika pale Mtoto wa kifalme anapotamani uhuru wa kutafuta mke yeye mwenyewe nje ya mila na desturi la taifa lake na kwenda Amerika na rafiki yake Semmi.
Akeem baada ya kufika Amerika akamua kujibadilisha na kugawa mali zake zote kwa omba omba na kuwa mtu wa kawaida kabisa ili kutafuta mwanamke atakaye mpenda kwa kila hali.
Akeem kama mtoto wa kifalme hajui kufanya chochote wala hakuwahi kujitegemea katika maisha yake na ndipo yeye na rafiki yake wakamua kwenda kuomba kazi katika mgahawa mdogo wa McDonald na ndipo anakutana na mtoto wa boss wake (Lissa )ambaye anatamani kuona mwanae akiolewa na mtu tajiri.
Vituko vinaanza pale Akeem na Lissa wakipendana sana huku wazazi wa Lissa wakipinga mapenzi yao kwa kutokujua Akeem ni Mwana wa Mfalme.
Muda unaenda ndipo baba yake Akeem Jaffe Joffer (James Earl Jones) anapoamua kwenda kumchukua Akeem na ndipo wazazi wa Lissa kugundua kuwa Akeem ni mtoto kutoka familia ya kifalme na ndiye atakuwa mrithi wa Taifa la Zamunda.
Akeem anarudishwa kwao akiwa mnyonge kwa kujua hatakuwa na Lissa na kwenda kuozeshwa na mwanamke mwengine wa kiafrika.
Siku ya harusi Akeem akiwa mnyonge anashangaa kumuona bibi harusi wake aliyejifunika ni Lissa furaha inazidi kuwa kubwa na ndipo anamua kujiuzulu akikataa maisha ya kifalme na kutaka kuishi kama raia wa kawaida katika taifa hilo za Zamunda.
Baada ya miaka 33 Filamu hii inaendelezwa tena na kufanyiwa muendelezo wa pili pale wanapoonesha kumbe Akeem alipokuwa Amerika kabla ya kukutana na Lissa mkewe aliwahi kuwa na mwanamke mwingine waliokutana Club Leslie Jones.
Mwanamke huyo ana mtoto mkubwa wa kiume ambaye anatakiwa kwenda Afrika kwa baba yake kujionesha kama ni mtoto wake wa kweli na awe mwanafalme je familia ya Akeem itampokea mtoto huyo?.Ukitazama filamu hiyo utapata majibu ya visa vyote.