Lulu Diva atamani kuwa mama

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abasi maarufu kama Lulu Diva, ameonesha hisia zake za dhati kuhusu hamu yake ya kupata mtoto ambaye atampa faraja na kumtunza maishani mwake.
Lulu Diva amefunguka kuwa ni matamanio ya kila mwanamke kuwa na mtoto, kwani mtoto huleta furaha na maana katika maisha.
“Nilikuwa na mama yangu tangu zamani, lakini alitangulia mbele za haki. Binafsi, natamani sana kupata mtoto. Kwa kuwa mimi ni Muislamu, natakiwa kuolewa kwanza, lakini ukweli ni kwamba natamani sana kuwa mama,” amesema Lulu Diva.
Msanii huyo ameongeza kuwa anatamani kupata mtoto ambaye atamtunza baadaye, kama ambavyo yeye alimtunza mama yake hadi mauti ilipomkuta.
Pamoja na hilo, Lulu Diva anaamini kuwa kila kitu kina wakati wake, na Mungu atamjalia kupata mtoto kwa wakati wake.
Pia aliwataka watu kuacha kuwasema vibaya wanawake wanaotamani watoto, akisisitiza kuwa “wanaomsema Wema hawana hofu ya Mungu, kwani naamini sisi sote tutapata watoto kwa wakati wa Mungu.”