Ligi Kuu

Kwa kauli hii ya Mkude wamekwisha!

KIUNGO wa Yanga, Jonas Mkude amesema hana presha na mechi ya watani wa jadi (Kariakoo Derby) kwa kuwa ameshacheza mechi nyingi.

Amesema mechi hiyo ni kama unapokutana na timu nyingine ila kikubwa ni jinsi mchezaji anavyoamka na kuweka akili yake kuelekea mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Oktoba 19, Yanga wakiwa ugenini dhidi ya watani hao Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

“Binafsi nimecheza mechi nyingi za Dabi, sina presha, kwangu muda wowote hata nikitoka kuamka naipiga bila shida,” amesema Mkude.

Ameongeza kuwa mara nyingi mchezaji anapojipa presha anashindwa kucheza mchezo huo na inapokuja suala la mashabiki wengi kujitokeza uwanjani na zile kelele kumchanganya zaidi.

 

 

Related Articles

Back to top button