Michezo Mingine

Kundi la kwanza la TZ lawasili Paris

UFARANSA: KUNDI la kwanza la Timu ya Tanzania itayoshiriki Michezo ya Olimpiki nchini Ufaransa limewasili salama jijini Paris leo na tayari kwa michezo hiyo inayotarajia kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, 2024 katika jiji la Paris.

Kundi hilo la kwanza lina waogeleaji wawili, Sofia Latiff na Collins Saiboko na mwalimu wao Alexander Harrison pamoja na Daktari wa timu, Dkt Eliasa Abdallah.

Waogeleaji wataanza katika mashindano hayo mchezo wa kuongelea mashindano yataanza Julai 30, mwaka huu ambapo Saiboko atashindana katika michuano ya mita 100 Freestyle kwa wanaume na Sofia Latiff atashindana Agosti 3, ataongelea bwawa la mita 50 freestyle kwa wanawake

Mwingine aliyewasili leo Paris ni mwalimu wa mchezo wa Judo, Innocent Mallya, mchezaji wake, Andrew Mlugu (Kg 73), tayari yupo Paris kwa mwaka katika kambi maalumu ya mazoezi ya CRJ Centre iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC).

Mlugu ataanza kushindana Agosti 2, mwaka huu na wanamichezo wengine wanne wote wanariadha wa Marathon wako kambini Arusha wakijifua. Wanatarajiwa kuwasili Paris Augosti 7 na Marathon itakuwa Agosti 11.

Wanariadha hao wa Marathon ni Wanaume wawili, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, na wanawake wawili Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri.

Related Articles

Back to top button