Michezo Mingine

Poland kutuma wanajeshi 20 kulinda Olimpiki, Paris

WARSAW, Poland: NCHI ya Poland itatuma wanajeshi 20 kusaidia kulinda Michezo ya Olimpiki huko Paris nchini Ufaransa.

Mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Kitaifa ya Poland aliliambia shirika la habari la serikali PAP, wakati waandaaji wa mashindano hayo wakiwa katika harakati za kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto za kiusalama ambazo zinaweza kutokea.

Mji mkuu wa Ufaransa umekuwa katika hali ya tahadhari tangu mashambulizi ya kidini ya mwaka 2015 ambayo yaliua watu 130 na kujeruhi mamia ya watu.

Warsaw ilitangaza mwezi Machi kwamba kikosi cha wanajeshi wa Poland, wakiwemo washika mbwa, watakwenda Paris kama sehemu ya juhudi za kimataifa ili kuiwezesha Olimpiki kuwa salama.

Mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Kitaifa Jacek Siewiera aliiambia PAP kwamba Rais Andrzej Duda alikuwa ametia saini agizo kwa wanajeshi 20 wa Poland kusaidiana na wenzao wa Ufaransa.

Wafanyakazi wa Poland watatoa msaada katika mashindano hayo na wataendelea kukabiliana na matukio ya ugaidi kuanzia Juni 24 hadi mwisho wa Septemba.

Michezo ya Olimpiki itafanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, huku Michezo ya Walemavu ikitarajiwa kuanza Agosti 28 hadi Septemba 8.

Related Articles

Back to top button