Ligi Kuu

Sio ubingwa tu,hata ufungaji bora

SIMBA SC wameendeleza rekodi yao bora kwa kuichapa Namungo FC mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Mabao mawili ya penati kutoka kwa Jean Charles Ahoua dakika ya 48 na 72 yaliwapa Simba uongozi huku bao la tatu likifungwa na Steven Mukwala dakika ya 90, akiunganisha pasi ya Valentin Nouma.

Kwa mabao hayo, Ahoua sasa ana mabao 10 msimu huu, akilingana na mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora.

Katika michezo mingine ya ligi, Azam FC imetoka suluhu na Coastal Union, huku Mashujaa FC wakishinda 2-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Related Articles

Back to top button