
MSHAMBULIAJI wa Simba, Georgijevic Dejan amesema mkataba wake na klabu hiyo umevunjwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dejan ameandika: “Nathibitisha kwamba Mkataba wangu wa Ajira umevunjwa kutokana na ukiukwaji wa msingi wa Mkataba uliofanywa na Klabu. Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga mkono na upendo mlionipa.”
Hata hivyo klabu ya Simba haijathibitisha maelezo hayo ya Dejan.
Dejan raia wa Serbia alijiunga na Simba Agosti 7, 2022 akitokea klabu ya Domžale ya Slovenia.
Timu alizowahi kucheza kati ya 2010 na 2021 kabla ya kujiunga na Simba ni Zemun, Teleoptikm Spartak Subotica, Inđija, Voždovac, Ferencváros, Partizan, Irtysh Pavlodar na Velež Mostar.